Iran Yampa Mwanadiplomasia wa Sweden Saa 48 Kuondoka Nchini.
Iran imempa mwanadiplomasia mmoja wa Sweden saa 48 kuondoka nchini, katika hatua ya kulipiza kisasi baada ya Stockholm kumzuia mwanadiplomasia wa Iran kuendelea na shughuli zake nchini Sweden.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema Balozi wa Sweden mjini Tehran aliitwa wizarani Alhamisi na kuwasilishwa malalamiko rasmi kuhusu hatua na sera za Stockholm dhidi ya Tehran.
Iran pia imekanusha madai yaliyotolewa dhidi yake na Sweden, huku ikiikosoa nchi hiyo kwa kile ilichokitaja kuwa kuwahifadhi watu na makundi yanayoipinga Iran.
#utaridi
