Kivuko Cha Milioni 19 Arusha Faraja Kwa Wananchi

Baba Abby
0

 

Arusha

Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Samunge, Wilaya ya Ngorongoro, imekamilisha ujenzi wa Kivuko cha Rima, kinachounganisha kijiji hicho na eneo la Mojanane lenye mashamba.


Ujenzi wa kivuko hicho umegharimu Sh milioni 19.4, ambapo wananchi walichangia Sh milioni 14.4, huku Serikali ikikamilisha kwa Sh milioni 5 kupitia Mfuko wa Jimbo.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Samunge, Jonas Girobei, amesema kivuko hicho kimepunguza gharama za kusafirisha mazao kutoka shambani, ambapo awali gunia moja liligharimu Sh 10,000, lakini sasa linasafirishwa kwa takribani Sh 4,000.


Wananchi wameiomba Serikali kutengeneza barabara ya Samunge–Mojanane yenye urefu wa kilomita 5, hatua ambayo wanasema itapunguza zaidi gharama za usafirishaji na kuongeza faida kwa wakulima.


Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Nsahigwa George, amewapongeza wananchi kwa kushiriki ujenzi wa kivuko hicho na kuahidi kufanyia kazi ombi la barabara.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!