Kampuni Ya Sandaland Imetangaza Kuchukua Hatua Dhidi Waziri Wa Paul Makonda

Baba Abby
0

 

Paul Makonda

Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imetangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kauli iliyotolewa hadharani na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kuhusu jezi za Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.


Hatua hiyo imetangazwa kupitia tamko rasmi la kampuni hiyo, iliyosema kauli ya Makonda iliyotolewa Septemba 16, 2026 kupitia akaunti yake ya Instagram imeathiri jina, chapa, hadhi na uhalali wa bidhaa za Sandaland katika soko.


Katika ujumbe huo, Makonda alinukuliwa akisema: “Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi. Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu haina taarifa.” Ujumbe huo uliambatana na picha ya Naibu Waziri Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, akiwa amevalia jezi yenye mchanganyiko wa rangi ya njano, bluu, nyeusi iliyochanganyika na kijani.


Sandaland imesema kauli hiyo imezua taharuki na sintofahamu, huku ikidai kuwa tayari imesababisha madhara ya kiuchumi na kwa hadhi ya kampuni. Kampuni hiyo imeeleza kuwa ina mkataba halali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kutengeneza na kusambaza jezi za Taifa Stars, ambazo zimekwishatumika katika mashindano mbalimbali ya timu za taifa za wanaume na wanawake.


Kutokana na hali hiyo, Sandaland imesema haitanyamaza na inakusudia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kauli hiyo, ikidai kuwa ilitolewa kwa namna inayoweza kuichafua chapa yake. Kampuni hiyo pia imesisitiza kuwa imejenga jina na heshima yake kwa muda mrefu na ilipewa dhamana kimkataba ya kushughulikia jezi za Taifa Stars.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!