Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amewataka Wafuasi wa chama hicho kuendelea kuwa imara na kutokubali kugawanywa kwa maneno.
Akizungumza leo, Novemba 6, 2026, katika Makao Makuu ya CHADEMA, Heche amesisitiza umuhimu wa umoja na kuendelea kupambana, huku akiwashukuru Mawakili kwa kazi waliyoifanya.
“Muwe imara, tutasonga na tutatoboa, nawashukuru Mawakili, siyo rahisi na historia itawaandika vizuri, Wanachadema wenzangu Nchi nzima, tupambane na tusikubali kugawanyika, na hii ndiyo njia sahihi,” amesema John Heche.
