Albert Chalamila: Makanisa Na Misikiti Vizingatie Mipango Miji

Baba Abby
0

 

Chalamila

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema Makazi holela ni miongoni mwa sababu zinazochangia uchafu katika mkoa huo, huku akieleza mpango wa kushirikiana na taasisi za nyumba kuboresha Makazi na kuendeleza Mji.


Akizungumza kuhusu mpango huo, Chalamila amesema wamekubaliana kuanza utaratibu wa kununua maeneo kutoka kwa Wananchi kwa makubaliano ya hiari kati ya muuzaji na mnunuzi, ili kuyaendeleza, hususan katika Sekta ya Makazi.


“Moja ya kitu kinachopelekea uchafu mkubwa katika mkoa ni kuwa na squatter nyingi,” amesema Chalamila, akitolea mfano eneo la Magomeni ambako ujenzi wa maghorofa umeboresha mwonekano na kuwezesha eneo hilo kuchukua wakazi wengi zaidi.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!