Lady Jay Dee amemzawadia nakala ya kitabu chake "Diary ya Lady Jaydee" mwanamuziki mwenzie, Diamond Platnumz baada ya kukutana, kupata chakula cha jioni na kufurahi pamoja.
Jidee ameonekana akiweka saini yake katika nakala ya kitabu hicho na kumkabidhi Diamond, ambaye kwanza, ameonekana kumpongeza Kwa mafanikio na kuthamini mchango wa safari yake katika muziki. Pia Diamond ameeleza kuwa na hamu ya kukisoma kitabu hicho, na kwamba kina maana katika maisha na kazi zake yeye Diamond Platnumz.
Jaydee na Diamond, ingawa safari zao kimuziki zilitofautiana muda wa kuanza, lakini wote wameweza kuweka alama muhimu na ya kipekee katika tasnia ya muziki nchini na kuwa inspiration kwa wasanii mbalimbali chipukizi na hata ambao tayari wanafahamika.
