Jeshi la Yemeni limetoa taarifa rasmi likikanusha madai ya Saudi Arabia kuwa limepanga kushambulia mji mtakatifu wa Makkah.
Jeshi hilo limeyaita madai hayo ya Saudi Arabia kuwa ni "uzushi na udanganyifu" unaolenga kupotosha hisia za umma na kuchochea chuki dhidi ya Yemen katika eneo la Mashariki ya Kati.
Uongozi wa Yemen umesisitiza kuwa taarifa hizo ni mbinu ya propaganda inayotumiwa na Riyadh ili kutafuta uungwaji mkono wa kisiasa na kidini katika vita hivi.
Yemen imethibitisha kuwa inaheshimu maeneo matakatifu na kwamba operesheni zake za kijeshi zinalenga tu maeneo ya kijeshi ya adui, ikituhumu Saudi Arabia kwa kutumia uongo ili kuficha kushindwa kwao uwanjani.
