Linah Sanga: Nimejifunza Kutochanganya Kazi Na Mahusiano

Baba Abby
0

 

Nandy

Linah Sanga katika mahojiano amesema kuwa kipindi cha nyuma alichanganya kazi na mahusiano na baadaye ikampa changamoto katika kazi zake za muziki, hivyo amejifunza na kutotaka kurudia tena kosa hilo.


Aidha, Linah ameeleza kuwa miongoni mwa mambo muhimu aliyoshauriwa na Nandy baada ya kuanza kusimamiwa kikazi na lebo yake ya "African Princess", ni kutochanganya mapenzi na kazi. 


Akizungumza na Wasafi FM, Linah ameeleza kuwa Nandy alimshauri aweke juhudi katika muziki wake usiingiliane na mahusiano yake binafsi, akitolea mfano kuwa kama anatakiwa kuwa studio inabidi afike Kwa wakati sahihi kama inavyohitajika badala ya kutoa visingizio visivyo na umuhimu au vinavyohusiaba na mahusiano ya kimapenzi.


Hata hivyo, Linah amesema ushauri aliopewa ni mzuri, huku akifafanua kuwa makubaliano yao ya kikazi na lebo hiyo bado hayamzuii kuwa katika mahusiano na mtu, isipokuwa ajue kutenganisha kazi na maisha binafsi ya mahusiano.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!