Meli ya kivita ya Jeshi la Wanamaji la India imegongana na meli ya Pakistan, PNS Hunain, katika Bahari ya Arabia Kaskazini, takribani kilomita 220 mashariki mwa Oman, Septemba 15.
India imemuita mwanadiplomasia wa Pakistan kuwasilisha malalamiko, ikidai kuwa PNS Hunain iliikaribia meli yake kwa mwendo wa kasi na kwa namna “isiyo salama,” ikikiuka makubaliano ya mwaka 1991 yanayotaka meli za pande hizo kutenganishwa kwa angalau maili tatu za baharini.
India imesema meli yake haikupata uharibifu mkubwa. Vyanzo vya India vinadai PNS Hunain ilionekana ikielekea bandarini ikiwa imeharibika, lakini taarifa hiyo bado haijathibitishwa.
Pakistan bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.
