Yemen Yaitungua Ndege Ya Saudi Arabia Aina Ya F-15

Baba Abby
0

 



MA’RIB, YEMEN — Jeshi la Yemen linaloongozwa na Ansarullah limedai kuitungua ndege ya kivita ya Saudi Arabia aina ya F-15 iliyokuwa ikifanya operesheni katika anga ya jimbo la Ma’rib.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi hilo, F-15 ilitunguliwa kwa kutumia kombora la ardhini kwenda angani lililotengenezwa nchini Yemen. Amesema ndege hiyo ilikuwa ikitoa msaada wa anga kwa operesheni za kijeshi za Saudi Arabia katika eneo hilo.

Jeshi la Yemen pia limedai kuwa ndege nyingine za Saudi Arabia aina ya F-15 na Typhoon, zilizokwenda eneo hilo kutafuta mabaki ya ndege iliyotunguliwa, zililazimika kuondoka baada ya kukabiliwa na makombora ya Yemen.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!