Elon Musk Apata Hasara Kubwa Ya Dola Za Kimarekani Milioni 500

Baba Abby
0

 

Elon Musk

Wiki mbaya kazini! Siku chache tangu Elon Musk apate hasara kubwa kwa kuwekeza zaidi ya dola za Kimarekani milioni 500 kwenye uchaguzi nchini Marekani kukisapoti chama cha swahiba wake, Donald Trump na kuishia kufeli vibaya kwenye uchaguzi huo, mapya yamemkumba tajiri huyo wa dunia.

Kampuni ya magari ya umeme ya Tesla inayoongozwa na Elon Musk imetangaza mpango wa kupunguza na kusitisha uzalishaji wa magari aina ya Cybertruck katika kiwanda chake cha Austin, Texas, Marekani, kuanzia katikati ya mwaka 2027.

Ingawa Musk ametangaza kuwa hatua hiyo inalenga kutoa nafasi kwa uzalishaji mkubwa wa magari aina ya Cybercab, yanayotarajiwa kutumika katika huduma za usafiri wa magari yanayojiendesha bila dereva, wachambuzi wa masuala ya teknolojia na uchumi, wamedai kuwa sababu kubwa ni kufeli sokoni kwa magari hayo.

Hata hivyo, haijafahamika iwapo Tesla itahamishia uzalishaji wa Cybertruck katika kiwanda kingine au kusitisha kabisa utengenezaji wake. Mhandisi mkuu wa mradi huo, Wes Morrill, ameashiria kuwa teknolojia iliyotumika kwenye Cybertruck itaendelezwa kupitia mradi wa Cybercab.

Cybertruck ilipata umaarufu kutokana na muundo wake wa kipekee, lakini mauzo yake hayakufikia matarajio ya kampuni. Awali, Musk alikuwa ametabiri kuwa Tesla ingeweza kuzalisha magari hayo 500,000 kwa mwaka, jambo ambalo halijawahi kutimia.

Mkakati mpya wa Musk kwa sasa ni kuelekeza nguvu za Tesla katika magari yanayojiendesha na roboti zinazofanana na binadamu aina ya Optimus, badala ya kutegemea zaidi mauzo ya magari ya umeme.

Hata hivyo, huduma ya magari yanayojiendesha ya Tesla bado inapatikana katika miji saba pekee nchini Marekani, huku roboti za Optimus zikiwa bado katika hatua za uendelezaji wa teknolojia kabla ya kuanza kuuzwa.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!