Adaiwa Kujiuwa Baada Ya Mme Wake Kukosa Nauli Arusha

Baba Abby
0

 


#HABARI Tukio la kifo cha Jasmini Hamisi, mkazi wa Mtaa wa Murieti, Kata ya Murieti jijini Arusha, limeibua maswali baada ya kudaiwa kunywa sumu na baadaye kujinyonga, siku moja baada ya kumwomba mumewe nauli ya kwenda Singida kuwasalimia wazazi wake.


Inaelezwa kuwa Jasmini alimwomba mumewe, Hamisi Maulidi, nauli ya safari hiyo, lakini akaambiwa asubiri hadi hali ya kifedha itakapokuwa nzuri.


Ombi hilo la nauli limeelezwa kuwa miongoni mwa matukio yaliyotangulia kifo chake, ingawa bado haijabainika iwapo kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mazungumzo hayo na tukio hilo.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Jasmini alidaiwa kutumia sumu kabla ya kujinyonga, huku mazingira kamili yaliyopelekea kifo chake yakihitaji kufahamika zaidi.


Tutaendelea kufuatilia na kukufahamisha taarifa zaidi kuhusu tukio hilo hususan kutoka kwa jeshi la Polisi.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!