Bibi Harusi Afariki Ghafla Baada Ya Kufunga Ndoa

Baba Abby
0

 


Bi. Flaviana Hokororo biharusi amefariki dunia saa nne tu baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Clemence, Kijiji cha Nambaya, Masasi, mkoani Mtwara.


"Nimeumia sana kwa sababu mke wangu bado namuhitaji ndiyo kiungo cha familia yangu amenitengenezea familia.


Nilimwambia mke wangu mimi nakupenda sana, na nina nia ya dhati kabisa ya kufunga ndoa na wewe, nakuomba kwa kuwa lengo letu ni kufunga ndoa ebu tufunge ndoa hapa hapa kitandani kwa sababu sheria zinaturuhusu" Amesema Bwana Harusi ambaye amempoteza mke wake baada ya ndoa.


Flaviana alifunga ndoa akiwa amelazwa kitandani baada ya kuugua ghafla, huku Padre, bwana harusi na mashahidi wakikamilisha taratibu za ndoa chumbani akiwa amevalia shela.


Hata hivyo, muda mfupi baadaye hali yake ilizidi kuwa mbaya na kukimbizwa kituo cha afya, ambapo alifariki. Tukio hilo lilisitisha sherehe za ndoa na kuanza maandalizi ya mazishi.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!