Afungwa Na Askari Pingu Siku 3 bila Kufunguliwa

Baba Abby
0

 


Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Giles George Mkazi wa Wilaya ya Nkasi amelalamika kufungwa pingu na askari wawili wa Jeshi la Polisi (Majina Kapuni) kwa siku tatu Kuanzia Jumamosi Septemba 19 hadi Jumatatu Septemba 21, na Askari hao kutokomea kusikojulikana kwa kosa ambalo halitambui.


Inaelezwa kuwa Kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya kuhudumia Mifugo kwa Bosi wake ambaye ni Bwana Afya (Jina limehifadhiwa) tangu Julai mwaka huu, Hivi karibuni tabia ya Bosi wake ilibadilika kwani alikuwa akichukua watu wengine kufanya majukumu yake.


Anasema alipohoji ndipo Bosi wake akamwambia ikiwa amechoka kufanya kazi aondoke, Kijana huyo alipodai maslahi yake akaitiwa Polisi ambao walimfunga pingu na baada ya kugundua hana hatia yoyote walimuacha na Pingu wakidai hawana funguo za kumfungua.


Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa linawashikilia askari hao na Bosi wa Giles.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!