Cheka Tu Kufikia Tamati Oktoba

Baba Abby
0

 

Coy Mzungu

Baada ya miaka 9 ya kuwaburudisha mashabiki wa vichekesho, Cheka Tu Comedy Platform imetangaza kufunga rasmi safari yake.


Kupitia taarifa yao, Cheka Tu wameeleza kuwa Oktoba 2, 2026 watafanya onyesho lao la mwisho litakalojulikana kama “CHEKA TU: THE LAST DANCE.”


Wamesema uamuzi huo umetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, huku wakisisitiza kuwa hawakutaka kumaliza safari hiyo kimya kimya.


“Tulianza na nyinyi, na tunataka tumalize na nyinyi,” wameeleza.


Kwa kipindi cha miaka 9, Cheka Tu imekuwa sehemu ya burudani kwa mashabiki, ikiandaa maonesho, kuwapa jukwaa wasanii wa vichekesho na kujenga historia katika tasnia ya comedy.


Kupitia The Last Dance, mashabiki wamepewa nafasi ya mwisho ya kukutana na Cheka Tu, kucheka pamoja, kukumbuka safari ya miaka 9 na kusherehekea yote yaliyofikiwa.


“Cheka Tu ilikuwa ndoto yetu, lakini nyinyi ndio mlioifanya kuwa historia.” — Cheka Tu.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!