"Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande".
