Dudubaya: Ommy Dimpoz Anapigwa Miti

Baba Abby
0

 

Dudubaya

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Dudubaya, amezua gumzo kwenye Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva lililofanyika Arusha baada ya kuzimiwa kipaza sauti (Mic) akiwa stejini.


Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya Dudubaya kuhoji sababu za msanii Ommy Dimpoz kualikwa kwenye tamasha hilo, huku akieleza kuwa kwa mtazamo wake Ommy hakustahili kupewa nafasi hiyo na hata kutumia kauli kali dhidi yake.


Baada ya kuanza kutoa kauli hizo, Mic ya Dudubaya ilizimwa, jambo lililomkasirisha msanii huyo. Kwa hasira, Dudubaya alionekana kuitupa Mic hiyo chini, kisha akaamua kususia show na kuondoka stejini.


Tukio hili limeibua mjadala kuhusu uhuru wa wasanii kuzungumza wakiwa stejini, mipaka ya kile kinachoweza kusemwa kwenye matamasha, pamoja na mamlaka ya waandaaji na wadhamini katika kusimamia maudhui ya tamasha.


Na je, kuzima Mic ilikuwa njia sahihi ya kuzuia kauli hizo, au angepewa nafasi amalize kuzungumza? 


Je alicho Fanya Dudu ni sahihi?

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!