Mchungaji Jackson Shayo ametoa mtazamo kuhusu namna mwanaume anavyopaswa kutumia fedha katika mahusiano, akisema mchumba hapaswi kupewa fedha za matumizi wala kusomeshwa.
Kwa mujibu wa Mchungaji Shayo, wanawake anaowaona kuwa wanastahili kutumia fedha za mwanaume ni wanne pekee: mama aliyemzaa, dada aliyezaliwa naye, mke na binti aliyemzaa.
Amesema wanawake wengine wanapaswa kusaidiwa pale wanapohitaji, akisisitiza kuwa hilo linapaswa kufanyika kama sehemu ya msaada na matendo ya huruma, si wajibu wa matumizi.
Je yuko sahihi kwa kauli yake hiyo?
