Soma hapo chini Aina Ya Wanaume Wanaoweza Kutembea Na Mke Wako Kirahisi:
1. Wachora Tattoo
Hawa jamaa ni wastaarabu sana. Pamoja na changamoto za kushika mapaja, vifua, shingo nk, hiyo haina excuses. Ni “kazi ya sanaa.” Mpeleke wife wako ukiwa na amani kabisa, wengi sana bado wanazingatia weledi wa kazi (professionalism).
2. Trainer wa Gym
Ingawa muda mwingi trainers wanakaa vifua wazi, six-pack zinang’aa kama tiles, hiyo ni kuwapa motivation clients wao kuwa wanaweza pia. Trainers hawana budi, na inawalazimu kuwashika, kufanya “stretching” sometime, anakaba shingo au sehem flani ili clients aende sawa na zoezi — hizo ni sessions za mazoezi. Hawana mambo mengi hawa watu wana nidhamu ya hali ya juu.
3. Mchungaji/Nabii
Kazi za hawa watumishi nyingi ni kuwafungua na kuwapa ushauri na upako waumini wao. Wanawake wengi wameonekana kuwa wana vifungo, sometime deliverance inajitajika na inabidi wapelekwe hadi vyumba maalum vya kuwafungua vifungo vya ndani zaidi. Msiogope dini ina miongozo thabiti na imewapa nidhamu kubwa mno.
4. Daktari
Kuna mambo mengi katika miili yetu tunapopata magonjwa au wakati wa ujauzito.
Wanaofanya RX / uchunguzi sometime kuna body examination, sometime inamlazimu wife atoe nguo kwa uchunguzi zaidi.
Ingawa presha anaweza kuipata hapo hapo wife wako, usijali wewe kaa nje subiri majibu. Hata wife wako kama anatakiwa arudi clinic kesho, usijali unachotakiwa ni kujali afya.
5. Ex / Mzazi Mwenzake
Historia haifutiki, ni familia… ila sio lazima kiporo kipashwe. Majiko mengine hayawaki. Ex ni Ex, wameshaachana.
6. Jirani/Rafiki Tajiri
Majirani sometime tunasaidiana. Jirani wengi wanatufosia mazingira.
Kuna emergency zinatokea, labda mkichelewa kupata mshahara ili kulipa kodi, umeme umekata ghafla na hamuelewi, wife kumbe huwa anajiongeza anaongea na jirani yake waloshibana, anamsevh mnasogeza siku. Hayo ndo maisha
7. Rafiki wa Kiume (BFF)
“Ni best tu” wa wife wako. Huna haja ya kuwaza mbali coz hawezi kuwa hana mtu tofauti na wewe wa kubadilishana naye mawazo. Sometime anamliwaza na kumshauri, moyo wake unapovunika. Chill bro 💔.
8. Boss Wake
Anafanya kazi vizuri, overtime nyingi, posho nyingi = huo ni UTARATIBU TU wa ofisi kuongeza ufanisi.
Maboss wengi wamenyooka sana. Ukiingilia kibarua chake kitapotea na mtashindwa kusaidiana majukumu ya kifamilia
9. Mabaunsa & Bar Maid Bros
Anamhudumia vizuri, wife anakunywa na kula anachotaka au kupenda na huduma ya high standard. Mara nyingi anainjoi kupata huduma hapo. Na gharama sio kubwa. Hakuna asiyependa huduma nzuri.
10. Wapiga Picha
Hiki ni kizazi cha mapicha picha na posts. Mpiga picha: “Angalia huku, smile kidogo… geuza kiuno.” Picha inatokaje kali sasa? Kama ni mjasiriamali anapush bidhaa online, maybe magauni kama ya Niffer, maokoto hapo uhakika. Picha haina uhusiano na chochote, please bro calm down.
11. Bodaboda
Hawa ndio heroes wetu. Wife mara nyingi ana “Boda wake special yuko on time”, ukizingatia mabasi nayo jau kinomaa.
Sometime hata buku ya boda hana kwa mda huo, anafosi kwa boda anajua atalipa vipi au atalipa tu mbeleni huko. Hawa tuwape maua yao, wanasevu sana mizinguko yao sokoni, saluni nk.
Mapenzi sio karantini ya kumfungia mtu sako mbali na dunia. Uaminifu na mipaka ndio ulinzi wa kweli. Otherwise bro utateseka, utapata magonjwa ya moyo ukikaa kuwaza sana.
