Soko Lateketea Kwa Moto Mwanza

Baba Abby
0

 

Mwanza

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeunguza sehemu ya Soko la Mbao Sabasaba, lililopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi kwa wafanyabiashara.


Moto huo ulizuka majira ya saa nane usiku na kuteketeza mitambo ya kuchana na kuranda mbao inayomilikiwa na baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo.


Juhudi za kuuzima moto huo na kuzuia usienee katika maeneo mengine ziliendelea, huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na vyombo vya usalama vikifika eneo la tukio kutoa huduma.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni, amesema serikali itaunda kamati maalum ya kuchunguza chanzo cha moto huo na kubaini mazingira yaliyopelekea kutokea kwa tukio hilo.


Amesema kamati hiyo pia itatoa mapendekezo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kudhibiti matukio ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza katika soko hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!