Kilichofanywa leo ni uhuni ambao lengo lake ni kumuondolea credibility Heche na Chadema kwa ujumla. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (Sura ya 197), kifungu cha 70 na kanuni zake, inasema taarifa za kibenki za mteja ni siri na haziwezi kutolewa bila amri ya mahakama.
Hivyo, nyaraka za akaunti binafsi za Heche kuwasilishwa mahakamani bila ridhaa ya mahakama ni kinyume cha sheria na zinakosa uhalali. Ikiwa nyaraka hizo zilihitajika kwa ajili ya kesi, Jamhuri ilipaswa kuwasilisha kwanza maombi mahakamani na mahakama itoe amri kwa benki husika kutoa nyaraka hizo.
Lakini leo kimefanyika kitu tofauti. Zimeletwa nyaraka bila kufuata utaratibu wa kimahakama. Hiyo ni invasion of privacy. Ni sawa na Jamhuri kuleta sms unazochat na mpenzi wako, wakati Mahakama haijatoa kibali cha kuchunguza mawasiliano yenu. Ni uhuni tu.
Walioleta nyaraka hizo wamezitoa wapi? Wamepewa na nani? Na kwa malengo gani? Je benki imeshirikiana na waendesha mashtaka wa Serikali kutoa siri za mteja kinyume cha sheria? Na Mahakama imekubalije kupokea nyaraka zisizo na authentication?
Sheria ya Ushahidi (Evidence Act, Sura ya 6) inasema nyaraka zinazotolewa mahakamani lazima ziwe na uthibitisho wa uhalali wake. Sheria ya kanuni ya adhabu (Penal Code, Sura ya 16) inasema kupata nyaraka kwa njia isiyo halali ni kosa la jinai. Kwa lugha rahisi mawakili wa Jamhuri wametenda jinai kwa kuwasilisha nyaraka kwa njia isiyo halali. Kwahiyo Heche anaweza kuomba ushahidi wake uondolewe.
Mazwazwa wanaweza kushangilia kwa sababu aliyefanyiwa uhuni ni Heche, lakini kesho inaweza kuwa wewe na ukose wa kukutetea. Ikiwa wana uwezo wa kuingilia akaunti ya Heche kinyume cha sheria, watashindwaje kuingilia akaunti yako wewe Ashura wa Yombo Mwanagati?
Unajiona upo salama kwa sababu ni CCM? Ngoja nikukumbushe, wakati Ben Saanane anapotea, wana CCM walijiona wapo salama sana. Waliamini mambo ya kutekwa ni ya wapinzani tu. Lakini leo Polepole yuko wapi? Chonchorio yuko wapi? Historia inafundisha kuwa uhuni wa kisheria unaweza kumfika mtu yeyote bila kutarajia. Kwahiyo Dososo la Jamhuri dhidi ya Heche leo ni Batili
