Mrembo Dolly Restie amesema kuwa kwenye tangazo la majeans alilopewa na duka la Room of Jeans hakuwahi kulipwa milioni 35 kama alivyosema .
Dolly Restie anadai mpaka sasa anaidai kampuni na hakuwahi kulipwa milioni 35 kama vile alivyojinadi kipindi cha nyuma.
Dolly ameeleza kuwa mwezi wa kwanza alilipwa lakini mwezi wa pili hakulipwa na alipojaribu kuwapigia simu alikuwa hapokelewi simu zake na licha ya hivyo anaidai kampuni.
''Milioni ngapi mia hamsini nyinyi si wasanii mliwahi kushuti matangazo hiyo milioni 35 mnaona nilipewa kweli hakuna milioni 35 kwanza kilichotokea nimefanya kazi mwezi wa kwanza nilipewa hela mwezi wa pili mtu hapokei simu naidai kampuni '' Amesema Dolly Restie
