Mwanaume Akutwa Akiwalawati Mashoga Wawili Arusha

Baba Abby
0

 

Arusha

Mmiliki wa nyumba ya wapangaji iliyopo Kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, ambaye jina lake limehifadhiwa, amedai kuwafumania wanaume wawili wakiwa uchi ndani ya chumba kimoja.


Mmiliki huyo amesema tukio hilo limetokea baada ya mmoja wa wapangaji wake, anayetajwa kwa jina la Alex Kimario, kujifungia ndani ya chumba hicho pamoja na mwanaume mwenzake, hali iliyomfanya kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea.



Akizungumza na vyombo vya habari Septemba 21, 2026, mmiliki huyo amesema alilazimika kufungua mlango kwa nguvu baada ya watu waliokuwa ndani kukataa kufungua, ndipo alipodai kuwabaini wanaume hao wawili wakiwa uchi kitandani.


“...nikachukua shoka, nikamwambia nahesabu moja hadi tatu, waambie wafungue mlango... nikaufungua mimi hadi mwisho, kufungua pazia, namkuta huyo Alex yupo uchi kama alivyozaliwa, na mwenzie yupo uchi kitandani, wako wawili,” amesema.


Baada ya tukio hilo, Alex alizuiliwa na baadaye kuchukuliwa na Jeshi la Polisi, huku wanaume wengine wawili waliokuwa eneo hilo wakidaiwa kuondoka na hadi sasa hawajulikani walipo.


Uchunguzi wa Tukio hilo bado unaendelea kubaini uhalisia.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!