Niliachwa Na Mpenzi Wangu Kisha Nikalipishwa Milioni tano - Juma Ayo

Baba Abby
0

 


Mtangazaji wa vipindi vya michezo Tanzania Juma Ayo amefunguka kuwa wakati yupo Dodoma aliwahi kulipishwa kiasi cha shilingi milioni tano kutokana na kutaja mdhamini mwingine kwenye kipindi ambacho kulikuwa na mdhamini mwingine ambaye alipaswa kumtaja.


Juma Ayo ameeleza kuwa sababu iliyompelekea kufanya hivyo ni kutokana na maumivu ya kuachwa na mpenzi wake hivyo hakuwa sawa akajikuta anaharibu kazi yake.


''Wakati nilikuwa nafanya kazi dodoma mimi niliwahi kulipishwa fedha pale redioni kwasababu kipindi ulichoniacha nilikua nafanya kazi mpaka naharibu mimi nilienda kwenye kipindi nikasema tumekuwa sponsored na kampuni nyingine nikatangaza kampuni nyingine nikapewa invoice ya milioni 5'' Amesema -uma Ayo

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!