Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele (Steve Nyerere), amewasifu viongozi wakuu wa chama cha upinzani cha CHADEMA, Tundu Lissu na Godbless Lema, kwa hatua yao ya kuonesha utu na ukomavu mkubwa wa kisiasa baada ya kutuma salamu za ramiirambi kufuatia kifo cha Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hatua hiyo imekuja kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo Tundu Lissu, akiwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya uhaini, aliwasihi wafuasi na viongozi wenzake kufikisha salamu zake za pole kwa Rais Samia na wafiwa wote akisema, “Jamani, pelekeni pole zangu kwa wafiwa.” Kupitia mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema, ilielezwa kuwa Lissu alisisitiza kwamba kama asingekuwa gerezani, angesafiri mwenyewe hadi Zanzibar kwenda kumfariji Mkuu wa Nchi.
Akizungumzia uamuzi huo, Steve Nyerere ameeleza kuwa kitendo cha viongozi hao wa upinzani kuweka kando tofauti zao kali za kisiasa na kiitikadi na kusimama na Rais Samia katika kipindi hiki cha majonzi ni dhihirisho tosha la 'utu' na utamaduni halisi wa Kitanzania
