CHADEMA: Kuchukua hatua zidi ya wana harakati

Baba Abby
0

 


Mwanachama wa CHADEMA, Odero Charles Odero, ametoa rai kwa chama hicho kuchukua hatua za haraka na za dharura dhidi ya watu anaodai wamejivika sura ya wana harakati na kujaribu kuingilia uendeshaji wa chama bila kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.


Odero amesema baadhi ya watu hao hawana hata kadi za CHADEMA, huku wengine akidai kuwa wana uhusiano na vyama vingine vya siasa, lakini wamekuwa wakijaribu kutoa maelekezo na kushambulia viongozi wa chama kupitia mitandao ya kijamii.


Amesema kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ya kuwataka viongozi na wanachama wa chama hicho kutoa pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha mume wake inapaswa kuheshimiwa, akisema baadhi ya watu wamekuwa wakiwakosoa na kuwatukana viongozi wanaounga mkono kauli hiyo.


Odero amesisitiza kuwa CHADEMA ina malengo ya kisiasa ya kushika dola, tofauti na wanaharakati ambao, kwa mujibu wake, hawana malengo hayo, hivyo ameitaka chama kuchukua hatua ili kulinda umoja, heshima na uongozi wake dhidi ya kile alichokiita kuingiliwa na watu wasio na mamlaka ndani ya chama.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!