Tunapenda kusisitiza kuwa TFF haikuwa sehemu, wala kujua kabla maudhui ya Mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, na kuzungumzia jezi za timu ya Taifa.
Hivyo, TFF inaonya Sandaland Fashion Wear kuacha kutumia nembo hiyo katika maudhui ambayo hayana uhusiano wa kimkataba uliopo kati ya pande hizi mbili.
Vilevile TFF itaiandikia barua kampuni ya Sandaland Fashion Wear ili kupata maelezo ya kina kuhusu matumizi ya nembo hiyo katika Mkutano huo.
