Ukraine Kusitisha Mashambulizi Dhidi Ya Miundombinu Ya Nishati Nchini Urusi

Baba Abby
0

 


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema Kyiv iko tayari kusitisha mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati nchini Urusi ikiwa Moscow nayo itasimamisha mashambulizi dhidi ya miundombinu muhimu ya Ukraine.


Zelenskyy amesema Ukraine inahitaji uhakikisho kutoka kwa washirika wake, hasa Marekani, kwamba Urusi itaheshimu makubaliano hayo. 


Kauli hiyo imekuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kudai kuwa Urusi na Ukraine zimekubaliana kusitisha mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya kila upande. Hata hivyo, Zelenskyy amesema hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa bado. 


Zelenskyy amesema kusitishwa kwa mashambulizi kunapaswa kuwa kwa muda mrefu, kuaminika na kuleta manufaa halisi kwa raia, huku akisema bado hajaona dalili za kutosha kwamba Urusi iko tayari kumaliza vita.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!