Mapigano yameripotiwa kati ya vikosi vya serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF) katika eneo la Afar, kaskazini mwa nchi hiyo.
Vyanzo viwili vya misaada vimeiambia AFP kuwa mapigano hayo yametokea katika maeneo ya Abala na Erebti, huku chanzo kimoja kikisema yalianza usiku wa kuamkia Jumatano.
Chanzo hicho kimesema huenda mapigano hayo yakaenea, huku lori la chakula likitumwa kuwasaidia watu waliokimbia makazi yao. Idadi ya waliojeruhiwa au kuuawa bado haijajulikana.
Wakati huohuo, Ethiopian Airlines imesitisha safari zake kwenda Mekelle, Shire na Axum kutokana na hali ya usalama katika eneo la Tigray.
Mvutano umeongezeka baada ya TPLF na makundi mengine sita yenye silaha kutangaza muungano wa kuipinga serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.
