Mwanamitadao Carry mastory amedai kuwa Hamisa Mobetto amemfungulia kesi akimtaka amlipe fidia ya Sh600 milioni.
“LEO nimeamini msemo wa wahenga, ‘Sura sio Roho.’ September 2026, Hamisa Mobetto amenifungulia kesi ya madai mahakamani, kutaka nimlipe fidia ya Milioni 600 kwa video clip ya mwaka 2023, ambapo bado nilikuwa shabiki yake. Yaani kama ilikuwa kesi kipindi hicho, angeifungua mwaka huo huo, ila alikaa kimya miaka mitatu. 😳ðŸ˜
“Nililia sana usiku kucha. Sijalia kwa sababu ya kesi au kudaiwa Milioni 600, hapana. Nyie Watanzania ni mashahidi jinsi gani nimepambana na huyo dada. Oh my God! Zaidi ya miaka 8 bila malipo ya aina yoyote, hata kuniambia, ‘Carrymastory, chukua 600 hii unywe soda.’
“Hajawahi kunisapoti kwa chochote, hata kusema, ‘Nakupa exclusive interview izidi kukupandisha.’ Na wewe tena vijana wangu wakimuomba interview ajibu tu yanayoendelea mtandaoni, yani mpaka umpate ni kwambinde, licha ya kuwa shabiki yake namba moja.
“Aise, ubinadamu kazi sana. Nadhani labda anaona kufika hapo ni kwa nguvu zake, sina mchango wowote, mpaka kuthubutu kukaa na meneja wake na mwanasheria kuniandikia barua ya kunidai Milioni 600.
“Huyu dada hapa Insta nimepigana vita yake kubwa sana. Tumetukanwa pamoja, tumeonekana wachafu wote baada tu ya video zake na Diamond kuvuja kipindi hicho akiwa na Zari kwenye mahusiano.
“Nilipigana hii vita mpaka ikaonekana ni jambo la kawaida, tukashinda, kwasababu mimi ndiyo shabiki pekee niliyebaki upande wake na nina followers wengi. Mpaka leo hii anaonekana mtu. Sijawahi kumpambania star yoyote hivi.
“Asilimia 80 ya wanawake Watanzania walikuwa wanamchukia kwa hizo video. Mnakumbuka hii vita? Kweli..?
“Hiyo tabia haiwapendezi wengi, ila nilisimama naye. Leo hii kasahau kabisa. Dah, hii kitu IMENIUMA SANA.
“Miaka yote nimekuwa nikipambana kusema Dylan ni mtoto halali wa Diamond. Leo kisa Juma tu, eti video clip hata sekunde 30 haifiki, inafuta miaka 8 yote ya mimi kumpambania. Naandika huku natokwa na machozi. ðŸ˜
“Dah, aise, hakujawa na support yoyote aliyewahi kunipa huyo dada, na sikuona vibaya. Nilifanya tu kwa mapenzi. Kweli, tenda wema uende zako.
“Msione najiweka mbali na mastaa wa Bongo wengi, hawana shukrani. Wanadhani wao ni lazima uwasapoti. Ukimuona staa anapenda mashabiki zake na kuwaweka karibu, huyo mheshimu.”
ameandika Carrymastory.
