Binti Auawa Manyara Kwa Kuchomwa Kisu Tumboni

Baba Abby
0

 


Binti mwenye umri wa miaka 15, Elisifa Santueli Petro, aliyemaliza darasa la saba hivi karibuni, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni katika Kitongoji cha Mandi Magharibi, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.


Tukio hilo linahusishwa na unyang'anyi wa simu, ambapo majeruhi alipoteza maisha mara baada ya kufikishwa zahanati kupatiwa matibabu.


Mtuhumiwa anayetajwa kutenda kosa hilo na kutoroka ni kijana aitwaye Abeli Tembo Geje, mkazi wa Kijiji cha Gocho, Wilaya ya Hanang.


Mwenyekiti wa kitongoji hicho ameeleza kuwa wawili hao walionekana kufahamiana kabla ya tukio, na simu inayodaiwa kuchukuliwa kwa marehemu ilikutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambaye bado hajulikani alipo.


Familia ya marehemu imetoa wito kwa Serikali kuingilia kati ili kuhakikisha mtuhumiwa anapatikana na kuwajibishwa kisheria, huku Jeshi la Polisi likiwa limeanza uchunguzi na msako mkali wa kumnasa mkosaji huyo.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!