Mwanamke Wa Kenya Ahukumiwa Viboko 100 Saudi Arabia

Admin
0

 


Mfanyakazi wa nyumbani kutoka Kenya, Esther Wanja Muthoni (40), ambaye amekwama nchini Saudi Arabia, amehukumiwa kuchapwa viboko 100 baada ya Mahakama ya Riyadh kumtia hatiani kwa kosa la kufanya ngono nje ya ndoa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti la The New York Times, Muthoni alihukumiwa mwezi Oktoba 2026, huku hukumu hiyo ikiongeza ugumu katika juhudi zake za kurejea Kenya akiwa na Mwanaye, Abudy, aliyezaliwa Agosti 2025.

Muthoni, ambaye amekuwa akijaribu kurejea nyumbani kwa zaidi ya mwaka mmoja, amesema anaogopa adhabu hiyo na hana uhakika kama ataweza kuivumilia.

Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi nchini Saudi Arabia kupitia Kampuni ya Maharah Human Resources kabla ya kupata ujauzito kutokana na uhusiano wake na Mwanamume raia wa Misri.

Baada ya kujifungua, alikabiliwa na changamoto za Makazi na upatikanaji wa nyaraka za Mtoto wake, hali iliyochangia kuendelea kwake kukwama Nchini humo.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!