Binti aliyefariki dunia akiwa kwenye chumba cha kupanga (geto) jijini Arusha, ametambuliwa rasmi na ndugu zake kuwa ni Lucia Paul, aliyekuwa na umri wa miaka 17 na ambaye elimu yake iliishia darasa la saba.
Ndugu wa marehemu wameeleza kuwa Lucia alikuwa bado mdogo kiumri, huku wakisema hawakutarajia kujihusisha kwake na mahusiano katika umri huo.
Aidha, familia imeeleza kuwa marehemu alikuwa na changamoto ya kiafya ya kuanguka chini kila anapokasirika, hali ambayo imeongeza maswali kuhusu mazingira ya kifo chake.
Katika maelezo mengine, familia imedokeza kuwa huenda Lucia alikuwa akifanya kwa siri mahusiano hayo bila kuwafahamisha kikamilifu ndugu zake.
Hata hivyo, familia imesema bado inasubiri taarifa za daktari ili kufahamu chanzo halisi cha kifo chake, huku mazingira ya tukio yakisubiri ufafanuzi zaidi kutoka kwa mamlaka husika.
.jpg)