Mhubiri Paul Nthenge Mackenzie Ahukumiwa Miaka Mia Mbili Jela

Baba Abby
0

 


Mahakama Kuu ya Mombasa nchini Kenya imemhukumu Mhubiri Paul Nthenge Mackenzie kifungo cha miaka 200 jela baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya watu 191, wakiwemo watoto 190 na Mtu mzima mmoja, katika tukio la Shakahola.


Adhabu hiyo imetolewa leo, Novemba 6, 2026, na Jaji Diana Kavedza Mochache ambapo Mackenzie alikuwa ametiwa hatiani Oktoba 19, 2026, pamoja na wenzake 28 katika kesi hiyo iliyotikisa Kenya na kuvuta hisia za kimataifa.


Kifungo hicho kinajumuisha miaka 100 kwa mauaji yaliyotokana na kuwanyima Waathirika chakula na miaka mingine 100 kwa mauaji ya moja kwa moja, huku vifungo hivyo vikitakiwa kutumikiwa kimoja baada ya kingine.


Kesi hiyo ilibaini kuwa Mackenzie aliwaagiza Wafuasi wake kufunga hadi kufa kwa madai ya kwenda kukutana na Yesu, tukio ambalo liliibuka mwaka 2023 baada ya miili ya mamia ya Watu kufukuliwa katika makaburi ya kina kifupi kwenye Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!