Ashikiliwa Na Polisi Kwa Kukutwa Na Noti Bandia

Baba Abby
0

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamshikilia Dadi Kombo Hamad, mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Uzunguni Chamboni, Shehia ya Chamboni, Wilaya ya Micheweni, kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia 327 za Shilingi 10,000, zenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 3.27.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Septemba 22, 2026, upekuzi uliofanywa katika nyumba ya mtuhumiwa umefanikisha kukamatwa kwa vifaa na vitu mbalimbali vinavyodaiwa kutumika katika shughuli hiyo.


Vitu hivyo ni pamoja na karatasi 100 kwa ajili ya kutengeneza noti bandia, simu ndogo sita aina ya Tecno, simu janja mbili aina ya ZTE na Samsung, sarafu 100 za nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, mashine moja ya kusajili laini za simu, flashi moja pamoja na laini za simu 123 za mitandao mbalimbali.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!