Aliyekuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amemjibu Rais William Ruto akisema serikali yake imeendelea kumtaja na kumlaumu kwa changamoto zinazokabili nchi, badala ya kushughulikia masuala hayo.
Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Kitaifa la Chama cha Jubilee, Kenyatta amesema alikubali matokeo ya uchaguzi wa 2022 na kukabidhi madaraka kwa amani, akishangazwa na kuendelea kuhusishwa na matatizo ya serikali ya sasa.
Kenyatta pia amehoji kuitwa “Sponsor” na baadhi ya viongozi wa Kenya Kwanza kila anapotoa maoni kuhusu masuala ya kitaifa, akisema ana haki ya kueleza msimamo wake kama mwananchi na mwanasiasa.
Kauli hiyo imekuja wakati mvutano wa kisiasa kati ya Kenyatta na Ruto ukiendelea, huku Ruto akimtuhumu Kenyatta kwa kuhusika na shughuli za upinzani, madai ambayo yamekuwa yakipingwa na viongozi wa Jubilee.
