G7 Waitaka Iran Kusitisha Kuwapelekea Silaha Kundi La Wahouthi

Baba Abby
0

 

G7

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za G7 wameitaka Iran kusitisha kuisaidia kwa silaha na kuiunga mkono kundi la Wahouthi nchini Yemen, huku wakilaani mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya Saudi Arabia.


G7 imesema kuongezeka kwa mapigano kati ya Wahouthi na vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia kunatishia usalama wa nishati katika eneo hilo na duniani, pamoja na kuhatarisha biashara ya kimataifa kupitia njia muhimu za usafirishaji.


Mawaziri hao pia wamewataka Wahouthi kusitisha mara moja shughuli za kijeshi, vitisho na mashambulizi dhidi ya meli za kiraia, huku wakitoa wito wa kurejea katika mchakato wa kisiasa kwa nia njema ili kupunguza mvutano nchini Yemen.


Kauli hiyo imetolewa baada ya maelfu ya watu kuikimbia Yemen kufuatia mapigano na kutwaa maeneo ya pwani ya Bahari ya Shamu, ikiwemo maeneo yaliyo karibu na Mlango wa Bab al-Mandab, unaotumika katika usafirishaji wa bidhaa duniani.


Mawaziri wa Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani wameeleza pia kuwa wataendelea kuiunga mkono serikali ya Yemen na kuheshimu umoja, mamlaka, uhuru na uadilifu wa eneo lake. Taarifa hiyo imetolewa pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoendelea New York.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!