Askari Na Maabusu 12 Wamefariki Kwa Ajari Sekenke

Baba Abby
0

 


Watu 12 wamefariki na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari la Polisi lililokuwa limewabeba mahabusu na askari kugongwa na lori la mizigo katika eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.


Gari hilo lilikuwa na watu 13, wakiwamo mahabusu wanane na askari watano, waliokuwa wakisafirisha mahabusu kutoka Kituo cha Polisi Shelui kwenda Mahakama ya Wilaya ya Iramba iliyopo Kiomboi.


Kwa mujibu wa taarifa za awali, lori hilo lililokuwa limebeba mafuta ya dizeli kutoka Dar es Salaam kuelekea Rwanda lilifeli breki wakati likishuka Mlima Sekenke na kuligonga gari hilo la Polisi.


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, huku majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Iramba kwa ajili ya matibabu.


Taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zinatarajiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!