Raia Wa Uingereza Atekwa Malawi Na Watu Wasiojulikana

Baba Abby
0

 


Polisi nchini Malawi wametangaza zawadi ya zaidi ya Tsh milioni 40 kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa raia wa Uingereza, Nusrat Osman (47), anayedaiwa kutekwa nyara na watu wanne katika mji wa Blantyre.


Nusrat, mama wa watoto wawili na anayefanya kazi katika kampuni ya ukaguzi wa hesabu nchini Malawi, alitekwa mchana wa Ijumaa na watu hao waliokuwa wakitumia gari aina ya Nissan Dualis lenye rangi ya kijivu, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.


Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku wakitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia kumpata Nusrat au kuwabaini wanaodaiwa kuhusika na utekaji huo kuwasiliana na mamlaka.


Mamlaka zimeahidi kutoa zaidi ya Dola 17,000 za Marekani (Sh44 milioni), kwa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa Nusrat na kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria.


Hadi sasa, polisi hawajabainisha sababu ya kutekwa kwa Nusrat, huku wakisema watekaji hawajawasiliana na familia yake wala mamlaka za Serikali tangu tukio hilo litokee.


Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza imesema inafahamu taarifa za kutekwa kwa raia wake nchini Malawi na inaendelea kushirikiana kwa karibu na mamlaka za Malawi kufuatilia tukio hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!