Kijana Akutwa Amefariki Baada Ya Kupotea Kwa Siku 5

Baba Abby
0

 


Kijana mwenye umri wa miaka 28, Mussa Karani Sika, amekutwa amefariki dunia katika eneo la mlimani lenye vichaka, Kitongoji cha Sigino Chini, Kijiji cha Sigino, wilayani Babati, mkoani Manyara, baada ya kutafutwa kwa zaidi ya siku tano.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baba yake mzazi, Karani Sika, Mussa Sika, mkazi wa eneo la Endaberg/Nakwa, aliondoka nyumbani siku ya Jumatatu akielekea kumtembelea bibi yake.


Karani amesema kabla ya kuondoka, Mussa alieleza pia kuwa angeelekea kwa baba yake mdogo, lakini hakufika katika eneo hilo, huku simu yake ikishindwa kupatikana kuanzia siku hiyo.


Kutokana na kutopatikana kwake, baba yake mdogo, Abdi Sika, amesema ndugu pamoja na vijana wengine walianza msako wa kumtafuta.


Msako huo uliendelea hadi Jumamosi, Septemba 19, 2026, ambapo walifanikiwa kuuona mwili wake katika eneo la mlimani lenye vichaka.


Akizungumza kuhusu tukio hilo, Victor Molel, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sigino Chini, amesema alipokea taarifa kuhusu kupatikana kwa mtu aliyekuwa akitafutwa na baadaye alifika katika eneo hilo.


Aidha, imeelezwa pembeni ya mwili huo zilikutwa chupa mbili, ambapo moja inadaiwa kuwa na kimiminika kinachoweza kuwa sumu.Hali hiyo imeibua madai kwamba huenda Mussa alikunywa sumu na kufariki, ingawa chanzo cha kifo chake bado hakijathibitishwa rasmi, huku sababu iliyomfanya kufika katika eneo hilo pia ikiwa haijafahamika.


Jeshi la Polisi lilifika katika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi, huku likitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kutokujichukulia sheria mkononi, ambapo EATV imewasiliana kwa njia ya simu na RPC wa Mkoa wa Manyara kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo, hata hivyo simu yake haikupokelewa, Jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!