Bodi ya Filamu: Wamiliki wa Maktaba za Video Library Lazima Wasajiliwe

Baba Abby
0

 


Bodi ya Filamu Tanzania imewakumbusha wamiliki wa Maktaba za Video (Video Library) nchini kuhakikisha wanasajili biashara zao na kuhuisha leseni zao kwa mujibu wa sheria na kanuni za filamu.


Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na bodi hii leo Septmba 12, 2026, Bodi imeeleza kuwa ni kinyume cha sheria kumiliki, kuendesha au kufanya biashara ya Maktaba ya Video bila kuwa na leseni halali kutoka Bodi ya Filamu Tanzania, kwa mujibu wa Kanuni za Filamu na Michezo ya Kuigiza.


Aidha Bodi ya Filamu imewataka Wamiliki kuhakikisha kuwa ifikapo Septemba 30, 2026 wamiliki wa Maktaba za kuonyesha filamu wawe wamejisajili kupitia mfumo wa “Artist Management Information System (AMIS)” na kukata leseni, au kufika katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania kwa ajili ya taratibu za usajili na uhuishaji wa leseni.


Hata hivyo Bodi imewaonya wamiliki watakaoshindwa kutekeleza maelekezo hayo ndani ya muda uliowekwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kutozwa faini, kufungiwa biashara au kufikishwa katika vyombo vya kisheria.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!