WAAMUZI WA VAR WASIMAMISHWA BAADA YA KOSA LA KUMPA HAALAND BAO DHIDI YA MAN UNITED.
Waamuzi wa mfumo wa VAR, Matt Donohue na Msaidizi wake Blake Antrobus, wameondolewa kwenye orodha ya Waamuzi watakaochezesha michezo ya Ligi Kuu England mwishoni mwa wiki hii, kufuatia uamuzi wenye utata katika mchezo wa Manchester Derby.
Katika mchezo huo uliochezwa Jumapili, Manchester City iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United, kupitia bao la Erling Haaland ambalo awali lilikuwa limekataliwa kwa sababu ya kuotea kabla ya VAR kuingilia kati na kuliruhusu.
Baada ya mchezo huo, Pro Ref, chombo kinachosimamia Waamuzi wa soka England, kilikiri kuwa kulikuwa na “kosa la uamuzi” baada ya VAR kushindwa kuzingatia ushawishi wa Enzo Fernández, ambaye alikuwa katika nafasi ya kuotea wakati wa tukio hilo.
Kutokana na kosa hilo, Donohue na Antrobus hawatapewa majukumu ya VAR katika michezo ya Premier League ya wikendi hii. Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Waamuzi, Howard Webb, pamoja na timu yake ya uongozi, huku upatikanaji wao wa kuchezesha michezo ukitarajiwa kutathminiwa tena baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Ripoti pia zimeeleza kuwa kuna uwezekano wa wawili hao kukosa kuhusishwa na mechi za Manchester United katika siku zijazo, ingawa hilo bado halijathibitishwa rasmi na mamlaka ya Waamuzi.
Manchester City ilishinda mchezo huo wa Old Trafford kwa bao la Haaland na kuendeleza mwanzo wake mzuri wa msimu wa Premier League.
#UbuMedia
