"Napitia kipindi kigumu sana, Sina furaha yoyote kwenye maisha yangu, usiku silali nawaza furaha naitoa wapi kama wengine, sometimes watu wakiniona nje wanahisi ni mtu mwenye furaha ila ukweli ni kwamba nateseka sana Paula ndo anaelewa.
Mara watu wakuseme hivi mara vile, mara umri umeenda huna kitu cha maana, natamani muda Urudi Nyuma Nianze Upya Ili nifute kabisa makosa yangu ila ndo hivyo haiwezekani ila nashukuru tu bado Napumua nashukuru kwa hicho tu."
Ameongea Kajala kwa masikitiko makubwa huku akilia.
Wengi wamempa pole Kajala, na wengi wanahisi Kajala anaona umri umeenda huku hakuna cha maana alichofanya, na pia baadhi ya watu wanasema kinacho Mtesa Kajala ni mapenzi hajawahi kupata mtu Sahihi, yote hayo ndo yanafanya ajikatie tamaa ya maisha.
Ukweli ni kwamba Kajala anapitia Kipindi kigumu sana, na Harmonize anaweza kuwa ndo kachangia hii hali anayopitia Kajala kwa sasa.
