Watanzania Tumuombee Kiredio Hali Yake Ni Mbaya

Baba Abby
0

 


TUZIDISHE MAOMBI KWA AJILI YA KIREDIO


Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimwonyesha content creator Kiredio akiwa kwenye wheelchair imezua gumzo na kuwafanya mashabiki na watu mbalimbali kumuombea.


Katika video hiyo, Kiredio anaonekana akiwa amekaa kwenye wheelchair huku akisukumwa na mtu mwingine. Hali hiyo imeibua maswali mengi kuhusu afya yake na kinachoendelea kwa sasa.


Maimatha, mmoja wa watu maarufu kwenye mitandao ya kijamii, ameandika ujumbe wa kuomba watu kumuombea Kiredio. Kupitia ujumbe wake, amesema:


> “Hivi naota au inasemekana baada ya Kiredio kutapeliwa mill 60 akiwa China, hali ya ndugu yetu kiredio ilianza kudhoofu mpaka akakutwa na ugonjwa usiojulikana🥹 Nyieee😭🙏 Nini tena Kiredio wetu jamani… Mungu akufanyie wepesi, nakutafuta 🙌.”


Hata hivyo, taarifa kuhusu ugonjwa anaodaiwa kuwa nao Kiredio na madai ya kutapeliwa fedha milioni 60 nchini China bado hayajathibitishwa rasmi kwa taarifa tulizonazo.


Kwa sasa, mashabiki wameendelea kutoa ujumbe wa kumuombea na kumtakia afya njema na kupona haraka.


TUZIDISHE MAOMBI KWA KIREDIO. Mungu ampe wepesi na nguvu katika kipindi hiki.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!