"kwenye maisha yangu sikuwahi fikiria ipo siku itatokea Mimi kumaliza siku sijatongozwa, Leo hii Sitongozwi tena lakini miaka ya Nyuma nilikuwa natongozwa Kila dakika.
Hakuna kitu kibaya kama upweke, natamani sana kuolewa, natamani nipate mwanaume yeyote tu kikubwa anipende na awe na akili tu basi.
Kuna umri Fulani mwanamke unakuwa unajiona huhitaji kuolewa ila Kuna umri ukifika ndo utaelewa kuwa mwanaume ana nafasi kubwa sana, nateseka sana ni Bora tu niongee ukweli, najua umri wangu umeenda ila na Mimi nahitaji furaha".
Amesema johari muigizaji wa Bongo movie.
