Paula amedai kuwa mama yake amefunga kabisa ukurasa wa mahusiano na Rajabu, akisisitiza kuwa hakuna uwezekano wa wawili hao kurudiana tena.
Paula amesema licha ya kuheshimu maamuzi na hisia za mama yake, binafsi hakuwahi kufurahishwa na kitendo cha mama yake kurudiana mara kwa mara na Rajabu.
Kwa mujibu wa Paula, mama yake ameshafanya uamuzi wa mwisho na hata amesema hatarudiana tena na Harmonize, akidai kuwa ni bora aendelee na maisha yake akiwa single.
Paula pia ameongeza kuwa anatarajia kuja na interview maalum ya mama yake, ambapo ataeleza kwa undani matukio mbalimbali yaliyotokea tangu alipoanza mahusiano na Harmonize.
Paula akimdokeza rafiki yao Juma Lokole, mtangazaji wa Wasafi.
