Starlink Yafanikisha Upasuaji Kwa Kutumia Roboti Africa

Baba Abby
0

 

Starlink

Starlink yasaidia kufanikisha upasuaji wa kihistoria wa kwanza wa tele-robotic Afrika Magharibi


Nigeria imefanya historia katika sekta ya afya baada ya madaktari kufanikisha upasuaji wa kwanza wa tele-robotic (upasuaji wa mbali kwa kutumia roboti) Afrika Magharibi, kwa msaada wa mtandao wa Starlink.


Kulingana na taarifa zilizotolewa, daktari mpasuaji aliye karibu na Lagos (katika hospitali ya Redeemer’s Health Village huko Mowe, Jimbo la Ogun) alidhibiti roboti kwa mbali na kumtoa figo iliyokuwa na saratani kwa mgonjwa aliye hospitali ya Nisa Premier Hospital jijini Abuja, umbali wa takriban kilomita 500.


Upasuaji huo, unaojulikana kama robot-assisted right radical nephrectomy, ulifanyika Jumamosi jioni kwa kutumia mfumo wa roboti wa Toumai. Ulihudumiwa kwa ushirikiano kati ya Redeemer’s Health Village, RoboMed Global na Nisa Premier Hospital.


Profesa Obi Ekwenna-Davis, mtaalamu wa urology na transplantation na mwanzilishi mwenza wa RoboMed Global, aliongoza operesheni hiyo. Alisema mgonjwa yuko katika hali nzuri na anatarajiwa kuruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya saa 24.


Mtandao wa Starlink ulitumika kuhakikisha mawasiliano yasiyokatizwa kwa wakati halisi kati ya daktari na roboti, huku MTN ikiwa mbadala wa dharura. Operesheni ilichukua takriban saa tatu.


Wataalamu wanasema mafanikio haya yanaonyesha uwezo wa teknolojia ya kisasa kupanua upatikanaji wa huduma maalum za upasuaji nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla, na yanaweza kusaidia kupunguza wagonjwa wa matibabu nje ya nchi.


Hii ni hatua muhimu katika maendeleo ya afya barani Afrika.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!