Kijana Wa Murieti Arusha Auza Nyumba Ya Shangazi Yake

Baba Abby
0

 


Mwanaidi Ally, mkazi wa Mtaa wa Murieti Mashariki, Kata ya Murieti, jijini Arusha, ameomba mamlaka zinazohusika kuingilia kati baada ya kudai kuwa eneo na nyumba aliyojenga pamoja na mume wake, Kassim Issa Husein, zimeuzwa bila ridhaa yao.


Mwanaidi amesema yeye na mume wake walinunua eneo hilo mwaka 2012 na kuanza kujenga nyumba taratibu kulingana na uwezo wao.


Amesema Issa Abubakar, mtoto wa wifi yake, walimlea kama mtoto wao na baadaye wakampa hifadhi katika eneo hilo kwa kuwa hakuwa na sehemu ya kuishi. Amesema kijana huyo ambaye alipokuwa akimuona Kassim humuita mjomba, amegeuka na kudaiwa kuuza eneo na nyumba hiyo.


Mwanaidi amesema siku moja alipofika katika eneo hilo aliambiwa Issa Abubakar hayupo na ameondoka. Alipouliza kuhusu eneo na nyumba hiyo, alielezwa kuwa tayari vimeuzwa.


Amesema mauziano hayo yalifanyika bila ridhaa yao, wakati mume wake akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru na akiwa hawezi kuzungumza.


Mwanaidi amesema hadi sasa mume wake bado ni mgonjwa na hawezi kufanya chochote, hali inayomfanya ashindwe kuchukua hatua mwenyewe kuhusu suala hilo.


Ameiomba mamlaka zinazohusika kuchunguza suala hilo na kumsaidia yeye pamoja na mume wake kupata haki yao.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!