Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamemtaka Mwinjilisti wa Kanisa hilo, Mzee Agrey Mwanri, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuepuka kiburi na kuhakikisha anatumia nafasi yake kwa maslahi ya Watanzania.
Angalizo hilo limetolewa na Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo, pamoja na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Magharibi Kati, Dkt. Isaac Kisiri Laizer, wakati wa Ibada ya Shukrani ya Mwinjilisti Mzee Agrey Mwanri.
Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la KKKT Jimbo la Siha, mkoani Kilimanjaro, ambapo Mwanri alitoa shukrani kwa Mungu kwa mambo mbalimbali aliyomtendea katika maisha yake.
