Msanii wa Bongo Flava, Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya, amewashukuru Watanzania kwa kumchangia fedha za kulipa faini ya Shilingi milioni 3 aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Dudubaya amesema faini hiyo iliyolipwa na wasanii Madee, Babu Tale na Fid Q, badala ya kuitumia fedha alizokuwa amepanga kulipa, ameamua kuzigawa kwa watu anaowataja kuwa wanahitaji msaada wa matibabu.
Amesema fedha hizo atawapeleka kwa Mzee Zahir Zoro, baba wa Banana Zoro, pamoja na msanii Prof Jay na mama yake, ambao amesema wanakabiliwa na changamoto za kiafya za muda mrefu.
“Hiyo milioni tatu ambayo nilipanga kulipa faini, nitampelekea baba yake Banana Zoro, Mzee Zahir Zoro, ambaye ni mgonjwa wa muda mrefu, pia ndugu yangu Prof Jay ambaye pia ni mgonjwa wa muda mrefu, pamoja na mama yangu mzazi naye ni mgonjwa wa muda mrefu sana. Wote nitawapatia milioni moja moja. Hiyo ndiyo sadaka yangu,” amesema Dudubaya.
